Google yabadili muonekano wa Nembo yake

Haki miliki ya picha .
Image caption Google yaamua kwenda na kasi ya uhitaji wa huduma ya watumiaji wake

Google imebadili nembo yake mpya kwa ajili ya watumiaji wake.

Muonekano mpya wa nembo hii unaonekana kuwa wa rangi zenye kuvutia.

Google imesema mabadiliko haya, yalihitajika kwa sababu watumiaji wake wengi wanapatikana kwenye simu za mkononi kuliko tarakilishi.

Kampuni ya Google imesema muonekano wa Nembo hii mpya, ni mzuri kwenye vioo vya aina mbalimbali vya simu na vifaa vingine ambavyo watumiaji wake hutumia Google.

Google imetangaza mabadiliko ya mtandao wake wakisifu kuwa ni rahisi zaidi,yenye kupendeza,ya kirafiki nembo ya sasa ya Google imepambwa kwa rangi ya samawati, nyekundu, njano na kijani kibichi.