Nigeria kudhibiti wizi wa Mafuta

Haki miliki ya picha NCSIST
Image caption Ndege zisizo na rubani kukomesha wizi wa mafuta Nigeria

Nigeria ina mpango wa kutumia ndege ndogo zisizokuwa na rubani kudhibiti wizi wa mafuta ulio kithiri nchini humo na mabao unaofanywa kwa kutumia Meli.

Kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini Nigeria NNPC humo imesema kuwa ina mpango kukomesha wizi wa mafuta ndani ya miezi nane ijayo. Nigeria ni moja kati ya Nchi wazalishaji wakubwa wa mafuta barani Afrika,lakini cha ajabu ni kwamba haipati mapato kutokana na mafuta kutokana na wizi mkubwa unaofanyika na kulipotezea taifa mapato.

Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari ameapa kusafisha uozo katika katikaviwanda hivyo. Mafuta kwa Nigeria yanachangia kwa asilimia 70 pato la serikali na kuifanya Nigeria kuwa miongoni mwa mataifa imara kimapato. Ripoti ya wataalam wa uchumi wa Think tank ya mwaka 2013 inasema mapipa laki moja huibiwa kwa siku sawa na asilimia tano ya uzalishaji wa taifa hilo kwa siku. Kutokana na wizi huo mkuu mpya wa kampuni ya mafuta ya taifa ya NNPC Ibe Kachikwu amesema pia kuwa kampuni yake itashirikiana na jeshi la wana maji wa Nigeria kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo