Wahamiaji 2 wajificha ndani ya injini

Image caption Mtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari

Mhamiaji mmoja kutoka Afrika Magharibi, alifanikiwa kuingia eneo la Ceuta nchini Uhispania kutoka Morocco, huku akiwa amejikunja ndani ya injini ya gari na mwingine akiwa amejificha nyuma ya kiti cha gari moja aina ya Mercedes-300.

Maafisa wa polisi wa Uhispania waliwapata wawili hao siku ya Jumapili wakati wa msako wao wa kawaida katika kituo cha El Tarajal, karibu na mpaka wa Morocco.

Watu hao wawili kutoka Guinea, kwanza walipewa huduma ya kwanza, kwa sababu walikuwa wamekosa hewa safi ya kupumua.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari

Raia wengi wa mataifa ya Afrika kujaribu kuingia Cueta kama njia moja ya kufika Ulaya.

Gari hilo linasemekana kuwa na nambari bandia ya usajili.

Polisi nchini Uhispania wanawazuilia watu wawili raia wa Morocco waliokuwa ndani ya gari hilo, wakati iliposimamishwa.

Haijabainika mtu aliyekuwa katika injini alikuwa katika hali hiyo kwa muda gani kwa sababu alikuwa akivuta hewa ya sumu.

Image caption Mtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari

Hata hivyo wahamiaji hao wawili hawakuwa na stakabadhi zozote za kuwatambulisha na kwa sasa wanachunguzwa na polisi.

Ceuta na Melilla ni himaya ndogo mbili za Uhispania karibu na pwani ya Kaskazini mwa Afrika na Uhispania imeweka ukuta mkubwa ili kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ukuta uliojengwa na Uhispania

Ukuta huo umewalazimisha wahamiaji wengi kutumia mbinu zingine kuingia Uhispania kama vile kuogelea hadi bandari nyakati za usiku na hata kujificha ndani ya mikoba.

Mwezi uliopita mto mmoja kutoka Morocco alifariki baada ya kukosa hewa safi ya kupumua pale nduguye alipojaribu kumsafirisha kwa mkoba wake.