Besigye kutoana jasho na Museveni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kizza Besigye

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, sasa atapambana na rais Yoweri Museveni, kwa mara ya nne katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Bwana Besigye ameshinda uteuzi wa chama kikuu cha upinzani FDC, baada ya kumshinda mpinzani wake Mugisha Muntu.

Akihutubia wafuasi wake baada ya kuteuliwa, Besigye aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano wa kamati kuu ya chama hicho, kuwa huo ulikuwa mwanzo wa safari ngumu.

Amesema wangali na kibarua kigumu mbele yao na ana imani kuwa kwa pamoja watafanikiwa kutekeleza maazimio yao.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Museveni

Rais Museveni anataraji kuwa muhula wa tano licha ya upinzani kudai kuwa muda wake umemalizika.