Mwanajeshi apatikana na hatia ya dhuluma za ngono

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Ufaransa C.A.R

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mwanajeshi mmoja wa kikosi chake cha kutunza amani, nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, kutoka Ufaransa amepatikana na hatia ya kumdhulumu kimapenzi msichana mmoja.

Kumekuwa na madai kadhaa kuwa wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Ufaransa walihusika na kashfa ya kuhusika kimapenzi raia wa nchi hiyo kwa kuwahonga na chakula.

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja la kutetea haki za kibinadam, Zeid Ra'ad Al Hussein ambaye yuko ziarani nchini CAR, amethibitisha tukio hilo.

Amesema tukio hilo lilitokea mwaka uliopita na msichana hiyo alijifungua mtoto Aprili mwaka huu.