Liberia imefanikiwa kutokomeza Ebola-WHO

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtu aliyenusurika ebola

Shirika la afya duniani WHO, limetangaza kwua taifa la Liberia, limefanikiwa kutokomeza Ugonjwa wa Ebola kwa mara ya pili.

Mei mwaka huu shirika hilo lilikuwa limetoa tangazo kama hilo, lakini mwezi mmoja baadaye, mtu mmoja alipatikana na virusi vya ugonjwa huo.

Shirika hilo limesema wataendelea kufanya ukaguzi wa hali ya juu kwa siku tisini nchini humo, ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautatokea tena.

Mataifa jirani ya Guinea na Sierra Leona yangali yanaandisha idadi ndogo ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo.