Wajumbe wa FDC wakutana Kampala

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kizza Besigye akiwa na wafuasi wake

Wagombea wawili wanaotafuta tiketi ya kuwania urais kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, FDC, kwenye uchaguzi mkuu ujao wamewahutubia wajumbe wa chama hicho jijini Kampala.

Kiongozi mkongwe wa upinzani Kizza Besigye, amesema kinyang'anyiro hicho si cha kuteua mgombea atakayepambana na chama tawala cha rais Yoweri Museveni cha NRM.

Badala yake, Besigye amesema mchakato huo ni wa kuteua mgombea atakayeweza kukabili mifumo ya serikali ambayo inadhibitiwa kijeshi.

Meja jenerali mstaafu Mugisha Muntu, amesema Uganda, inahitaji kuunda taasisi zinazoweza kuwawekea mipaka viongozi, kwa kuwa nchi hiyo ina historia ya viongozi wanaopata uongozi na kusahau wajibu wao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Yoweri Museveni ambaye atakuwa mgombea wa chama tawala

Mshindi wa chma hiyo atapambana na rais wa sasa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na wagombea wengine wakiwemo aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Amama Mbabazi.