Besigye kupeperusha Bendera ya FDC

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kiongozi wa zamani wa FDC Kiza Besigye

Rais wa zamani wa Chama cha upinzani nchini Uganda, Forum for Democratic Change, FDC, Dokta Kizza Besigye ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera dhidi ya Rais wa sasa Meja Jenerali,Mugisha Muntu.

Besigye amejizoela kura 718 dhidi ya 289 katika uchaguzi uliokuwa vuta nikuvute uliofanyika jijini Kampala

Wajumbe wa FDC walikutana jumatano jijini Kampala kumchagua mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu mwakani.Rais wa sasa wa FDC Meja Jenerali Mugisha Muntu alipambana na Rais wa zamani wa

Chama hicho Kizza Besigye katika kinyang'anyiro hicho.

Dokta Besigye amejitosa tena kwenye mchakato wa Urais utakaofanyika mwakani.

Besigye sasa ataomba ridhaa ya wanachama kutoka muungano wa Vyama vya upinzani,TDA.