Zaidi ya watu 50 wahofiwa kuzama-Libya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji waliookolewa katika pwani ya Libya

Zaidi ya watu hamsini hawajulikani waliko baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuanza kuzama katika pwani ya Libya.

Msemaji wa shirika la kimataifa ya uhamiaji ameiambia BBC, kuwa wahamiaji wengine waliokuwa kwenye meli hiyo waliokolewa na wanajeshi wa majini wa Italia na wamepelekwa kisiwa cha Lampedusa.

Mwili wa mhamiaji mmoja pia uliopolewa baharini na kupelekwa katika kisiwa hicho.