Wahamiaji ni changamoto kwa Ulaya

Image caption Mtoto aokotwa ufukweni

Swala la wakimbizi na wimbi la wahamiaji katika nchi za ulaya linaendelea kutazamwa kwa karibu wakati maelfu ya watu wakisubiri kuruhusiwa kuingia katika nchi za jumuia ya ulaya.

Na siku ya Jumatano hali ilikuwa ya kusikitisha baada ya picha ya kijana aliyezama kuonekana akiwa katika pwani ya Bahari nchini Uturuki kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Siku ya jumatano, Waziri mkuu wa uingereza David Cameron alitetea uamuzi wa serikali yake akisema kuwa kuwapokea watu zaidi si ufumbuzi wa tatizo.

Badala yake, amesema ni muhimu kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo katika maeneo ambayo wahamiaji wanatoka, kama vile Syria.

Wakati huo huo mamia ya wahamiaji nchini Syria na wakimbizi walikwama kwa siku nyingine katika kituo cha reli mjini Budhapest,awali walionyesha hasira yao wakiandamana huku polisi wakishuhudia.