Austria leo kupokea wahamiaji 10,000

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji wakiwa kwenye basi

Austria imesema inatarajia kupokea wahamiaji wapatao 10,000 wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka Syria ambao wataingia katika nchi hiyo kutokea Hungary.

Usiku wa kuamkia leo wafanyakazi wa Shirika la misaada walipokea watu maelfu kwa maelfu baada ya nchi ya Hungary kutuma basi kuwachukua kutoka mpakani. Treni maalum zinawasafirisha kwenda Vienna.

Serikali ya Budapest imesema hakuna mabasi na treni zaidi ambapo makundi mengine ya watu wameanza kutembea kutoka mjini kuelekea kwenye mpaka wa Austria.

Ujerumani imesema nayo inatarajiwa wakimbizi wengi kuingia katika miji mbali mbali ya nchi hiyo.