Wakimbizi wawasili Austria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi wawasili Austria

Mamia ya wakimbizi walio na nia ya kuondoka nchini Hungary wameanza kuvuka mpaka kwenda nchini Austria ambapo wamepokewa katika kituo kimoja cha muda cha shirika la msalaba mwekundu wakionekana wamechoka lakini wakiwa na furaha.

Mabasi ya Hungary yaliwafikisha mpakani ambapo walitembea na kuingia nchini Austria.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakimbizi wawasili Austria

Msemaji wa polisi nchini Austria ( Werner Fasching) alisema kuwa karibu watu 3000 wanatarajiwa kuwasili saa chache zinazokuja.

Austria inasema kuwa wakimbizi hao wanaweza kuomba hifadhi nchini humo au waendelee na safari yao kwenda nchini Ujerumani ikiwa watapenda hivyo.