Israil yatakiwa kusaidia Wakristo zaidi

Wanafunzi wa shule za Wakristo wakiandamana Jerusalem Haki miliki ya picha AFP

Kumefanywa maandamano nchini Israel kuhusu madai ambayo waandamanaji wanasema ni ubaguzi dhidi ya shule za Wakristo nchini humo.

Wanaowaunga mkono wanasema shule hizo zinapata pesa kidogo sana za serikali ikilinganishwa na shule za kibinafsi za Wayahudi wenye msimamo mkali.

Maandamano hayo yalifanywa nje ya ofisi ya waziri mkuu mjini Jerusalem.

Wanafunzi na waalimu kutoka shule karibu 50 za Wakristo piya wamegoma hivi sasa ili kuichagiza serikali kuwapa msaada zaidi.