Tunisia yatangaza hali ya hatari

Polisi wa Tunis nje ya bunge baada ya shambulio kwenye makumbusho mwezi March 2015 Haki miliki ya picha

Wakuu wa Tunisia wameonya kwamba kuna tishio la mashambulio ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari katika mji mkuu, Tunis, na wamepiga marufuku magari katika baadhi ya barabara za katikati ya mji.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imesema taarifa za usalama zinaonesha kuna hatari kuwa maeneo muhimu ya mji yatalengwa lakini haikueleza zaidi.

Askari wa usalama wamefunga barabara kuu iitwayo Habib Bourguiba na barabara nyengine muhimu.

Tunisia tayari iko katika hali ya dharura, amri iliyoanzishwa awali mwaka huu baada ya wapiganaji kushambulia maeneo mawili ya watalii