Mashambulizi yapamba moto Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashambulizi yapamba moto Yemen

Ripoti kutoka nchini Yemen zinasema kuwa muungano unaongozwa na Saudi Arabia umefanya mashambulizi ya angani kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa, siku mbili baada ya shambulizi la waasi lililowaua wanajeshi 60.

Walioshuhudia walisema kuwa mashambulia hayo yalilenga ngome za waasi wa Houthi na vikosi vilivyo watiifuu kwa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.

Ripoti zingine kutoka hospitali za mji wa Sanaa zilisema kuwa zaidi ya raia 20 wameuawa kwenye mashambulizi hayo.