Ulaya kugawana wakimbizi 120,000

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji hawa kutoka Syria wamelalamikia hali duni katika kambi za wahamiaji nchini Hungary

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wameahidi kutumia mfumo mpya ya kugawana wakimbizi baina ya nchi za muungano wa ulaya.

Tangazo hilo lilitolewa na rais wa Ufaransa Francois Hollande, ambaye alisema kuwa nchi yake itawachukua wakimbizi 24,000.

Amesema kuwa chini ya mipango huo kutoka kwa tume ya ulaya, jumla ya wahamiaji 120,000 watagawanywa baina ya nchi za muungano wa ulaya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufaransa imesema itawachukua wakimbizi 24,000

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema kuwa nchi yake pekee haiwezi kusuluhisha hali iliyopo kwa sasa.

Hata hivyo waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban ameonya kuwa ugavi wa wahamiaji hauweza kufaulu chini ya mfumo wa sasa wa ulaya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ulaya kugawana wakimbizi 120,000

Wahamiaji elfu 20 wanakadiriwa kuingia Ujerumani mwishoni mwa juma na wengine wapatao elfu kumi na moja wanatarajiwa kufika nchini humo hii leo

Wakati huo huo Wahamiaji hawa kutoka Syria wamelalamikia hali duni katika kambi za wahamiaji nchini Hungary