Punda na farasi ni marufuku Nigeria

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jeshi la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram .

Kundi hilo limekua likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jimbo la Borno ndio kitovu cha vuguvugu la Boko Haram

Huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio katika vita vyake dhidi ya Boko Haram, kundi hilo linaripotiwa kukabiliwa na kibarua kigumu kupata mafuta ya kuweka kwenye magari yake kwa hivyo hutumia farasi kwa usafiri mbadala.

Lakini tayari kuna marufuku ya matumizi ya piki piki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake katika mashambulizi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kufuatia upungufu wa Mafuta Boko Haram imekuwa ikitumia punda na farasi kufanya mashambulizi yake

Pikipiki hizo zilirahisisha kutoroka kwa washambulizi , kwa hivyo kwa sasa kuna hofu kwamba marufuku ya sasa itadhoofisha zaidi uchumi wa maeneo ya vijijini na kuathiri maisha ya watu wa kawaida.

Punda hutumiwa kwa kusafirishia bidhaa na mara nyingi farasi huendeshwa katika tamasha za kidini na kitamaduni.