Bomu laua polisi 10 Uturuki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari lisilopenya risasi liliharibiwa kabisa

Takriban polisi 10 wa Uturuki wameripotiwa kuuawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya basi dogo mashariki mwa nchi hiyo .

Shambulio hilo limetokea siku mbili baada ya shambulio jingine dhidi ya magari ya kijeshi ya Uturuki kusini magharibi mwa nchi hiyo lililowauwa askari 16.

Image caption Ndege za kijeshi za Uturuki zimelipua maeneo yanayokaliwa na PKK Iraq

Maafisa wamewalaumu wapiganaji wa kundi la kikurdi la PKK kwa mashambulio hayo .

Wakati huo huo ndege za kijeshi za Uturuki zimefanya mashambiulizi zaid ya uvamizi dhidi ya ngome za PKK nchini Iraq.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shambulizi la awali liliwaua wanajeshi 16

Vyombo vya habari vya Uturuki na maafisa wa usalama wanasema ndege zaidi ya arobaini zimefanya mashambulizi na kuharibu handaki na maghala ya chakula ya PKK.