Aliyeiba mtoto miaka 18 iliyopita anaswa

Haki miliki ya picha VT Freeze Frame
Image caption Aliyeiba mtoto miaka 18 iliyopita anaswa

Mwanamke mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kuiba mtoto wa miaka mitatu kutoka kwa kitanda cha hospitali miaka 18 iliyopita.

Mwanamke huyo anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Cape Town Afrika Kusini.

Mtoto huyo wa kike alipatikana mapema mwaka huu katika shule moja ya upili akitumia majina tofauti.

Wazazi wa kibayolojia wa mtoto huyo, Celeste na Mourne Nurse waliunganishwa na mwanao baada ya mtoto huyo kujiunga na shule moja na dadake mdogo.

Baada ya kuwaona watoto hao wawili wakiwa wamefanana kama shilingi kwa ya pili,walimualika kwa kikombe cha chai nyumbani mwao na wakawaarifu polisi.

Image caption Wazazi wa kibayolojia wa mtoto huyo, Celeste na Mourne Nurse wameunganishwa mtoto wao

Vipimo vya vinasaba vilithibitisha utambulisho wa msichana ambaye alikuwa katika mikono ya mfanyikazi wa jamii.

Kwa hivi sasa mtoto huyo ametimia miaka 18 na anatarajiwa kukamilisha masomo yake mwaka huu.

Mwanamke anayedaiwa kuwa 'mamake' kwa maisha yake yote kwa sasa anakabiliwa na kosa la utekaji nyara, wizi na kukiuka sheria za watoto.

Ripoti ya IOL imesema mwanamke huyo bado hajajibu mashtaka.