Enzi ya Malkia Elizabeth ya miaka 63 !

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Malkia Elizabeth

Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ametimiza miaka 63 katika enzi.

Huo ni muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.

Alitawazwa kuwa malkia akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Image caption Alipotawazwa

Mara ya kwanza alipofahamishwa kuwa ndiye atakayekuwa malkia wa Uingereza alikuwa nchini Kenya .

Haki miliki ya picha
Image caption Akiwa na mumewe

Alikuwa katika ziara rasmi nchini Kenya akiwa na mmewe Philip wakati huo akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Image caption Malkia Elizabeth

Walikuwa wakikaa katika hoteli ya Treetops na jioni moja ikatangazwa kuwa babake amefariki akiwa usingizini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Malkia Elizabeth afisini

Na hapo akawa Malkia lakini hakuambiwa habari hizo hadi alasiri siku iliyofuata.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Malkia Elizabeth anawapenda mbwa

Mmewe alimpeleka katika ikulu ndogo ya Sagana na kumpa habari kwamba sasa ndiye malkia wa Uingereza.

Sasa miaka 63 baadaye Malkia anawashukuru sana wote waliomtumia ujumbe wa heri njema.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Malkia Elizabeth akipokea salamu

''Nawashukuru sana''

Haki miliki ya picha AP
Image caption Malkia akiwa na mumewe Prince Phillip

Akizungumza karibu na mpaka wa Scotland Malkia Elizabeth 89 alisema ni heshima kubwa kwake kuendelea kuwahudumia waingereza.

Image caption Malkia Elizabeth ameweka rekodi ya kutawala kwa kipindi kirefu zaidi cha miaka 63

Malkia Elizabeth amehudumu kwa siku 23,226 , yaani miaka 63 .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Malkia Elizabeth amehudumu kwa siku 23,226
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wengi wamesifu kwa unyenyekevu wake

Viongozi wengi wamemsifu kwa unyenyekevu wake .