Mataifa ya Ulaya sharti yawapokee wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jean Claude Juncker

Rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker, ametoa wito kwa watu barani ulaya kujitolea na kuonyesha utu na usawa kwa wakimbizi wanaoingia barani ulaya.

Junker amesema kwa licha ya muungano wa ulaya kutokuwa katika hali nzuri kiuchumi, ulaya inaonekana kama eneo salama na la matumaini kwa watu wengi kutoka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mataifa ya Ulaya sharti yawapokee wahamiaji

mashariki ya kati.

Akilihutubia bunge la ulaya bwana Junker alizitaka nchi za muungano wa ulaya kuwapa makao wakimbizi 160,000 wanaogawana kama sehemu ya mpango wa lazima baina ya nchi za ulaya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji walikurupuka Hungary

Mapema mpango huo ulioonekana kuwa bora ulipingwa vikali na baadhi ya nchi za muungano huyo.

Sasa mpango mwingine utajadiliwa kwenye mkutano wa mawaziri wa nchi za muungano wa ulaya siku ya Jumatatu.