Hakimu ataka Rais Guatemala ajibu shtaka

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa zamani wa Guatemala Otto Perez Molina

Rais Perez Molina alijiuzulu urais wiki iliyopita na anashikiliwa jela akisubiri kusikilizwa kwa madai ya kutumia mamilioni ya dola za wanawanchi kwa rushwa.

Molina akana tuhuma hizo. Viongozi wakubwa wengi wa kisiasa wamehusika katika kashfa hiyo.

Bunge la nchini Guatemala limemwapisha makamu wa rais Alehandro Maldonado, mpaka rais mpya atakapo chukua madaraka hayo mwezi januari.

Muigizaji wa vichekesho, Jimmy Morales, alishinda kura nyingi katika uchaguzi siku ya Jumapili lakini hazikutosha ili kuepuka kurudiwa kwa mwezi ujao.)