Wahamiaji wakurupuka Hungary

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji wakurupuka Hungary

Mamia ya wahamiaji wamevunja vizuizi vya polisi katika kivukio cha mpaka kati ya Serbia na Hungary.

Tukio hilo lilitokea karibu na mji wa Hungary wa Roszke ambapo wahamiaji hulazimika kungoja katika kituo kimoja kabla ya kupelekwa kati kituo cha ujasili kilicho karibu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hungary inakadiria kuwa zaidi ya watu 160,000 wamevuka mpaka wake mwaka huu

Mwandishi wa BBC eneo hilo anasema kuwa wakimbizi hao hawataki kusajiliwa nchini Hungary na wana lengo la kutembea hadi mjini Budapest kabla ya kusafiri kwenda maeneo wanayoyataka nchini Austria na Ujerumani.

Hungary inakadiria kuwa zaidi ya watu 160,000 wamevuka mpaka wake mwaka huu.