Ubakaji:India inamchunguza raia wa Saudi A

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ubakaji:India inamchunguza raia wa Saudi A

Polisi nchini India wanafanya uchunguzi kufuatia madai kuwa afisa mmoja mfanyikazi wa ubalozi wa Saudi Arabia aliwabaka wafanyikazi wawili wa nyumbani raia wa Nepal nyumbani kwake karibu na mji mkuu Delhi.

Wanawake hao waili waliwaambia polisi kuwa walibakwa.

Aidha wanadai kuwa walinyimwa chakula na kushikwa mateka kwa miezi kadha baada ya kuondoka nchini Nepal kwenda kumfanyia kazi afisa huyo.

Ubalozi wa Saudi Arabia umekanusha madai hayo.

Maelfu ya wanawake kutoka nchini Nepal husafiri kweda nchini India na mashariki ya kati kufanya kazi za nyumbani.

Mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa wa wahudumu hao wa nyumbani huteswa sana mikononi mwa waajiri wao.