Soko la hisa la Japan limepata faida kubwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Soko la hisa la Tokyo nchini Japan limepata faida

Soko la hisa la Tokyo nchini Japan limepata faida zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka saba.

Soko hilo limesema kuwa faida hiyo imepanda kwa kiwango cha asilimia saba nukta saba .

Masoko mengine ya hisa katika bara Asia pia yamerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuuza hisa kupita kiasi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe

Hapo awali yakisaidiwa na faida iliyopatikana kwenye soko la hisa la Marekani la Wall Street .

Matumaini zaidi yametolewa katika kauli ya ukuaji wa kiuchumi kutoka kwa waziri mkuu wa Japan kutokana na biashara zinazoendeshwa kupitia bahari ya Pacific.