Mpango wa kutega mabomu watibuliwa Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wa Kenya walipokuwa wakipambana magaidi katika Chuo Kikuu cha Garisa

Wanaume watatu wamakamatwa mjini Nairobi nchini Kenya baada ya mtu mmoja kuzuiwa wakati anajaribu kuingia katika jengo la maduka akiwa na kifaa cha kilipuzi katika mkoba wake.

Kifaa hiko kiliharibiwa na polisi wa kitengo cha kutegua mabomu nchini kenya.

Shuhuda anasema watu hao watatu walisimamishwa na walinzi wa usalama wakiwa wanajaribu kuingia katika jengo moja la maduka la Garden city Mall kwenye kitongoji kimoja Nairobi.

Mmoja wa wanaume hao alikataa kukaguliwa hivyo ilibidi walinzi wamdhibiti wa kumpiga ngumi.

Milipuko iligunduliwa katika mkoba wake.

Wateja na wafanyakazi wa maduka hayo waliondolewa na kifaa hicho kiliharibiwa na kitengo maalum cha kudhibiti mabomu.

Polisi anasema wanaume wote watatu wanaoshukiwa kuwa ni raia wa Kenya wamekamatwa.

Inaaminiwa kuwa bomu hilo ni kilipuzi kidogo chenye betri na kilichounganishwa kwenye simu ya mkonon ambayo ingetumia kulipua bomu hilo.

Miaka miwili iliyopita watu 67 waliuawa baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuvamia maduka ya Wastegate mjini Nairobi.