Mwandishi wa habari auawa Pakistan

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shambulizi hilo ni la tatu dhidi ya waandishi habari katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Polisi nchini Pakistan wanasema kuwa watu wenye silaha wamemuua kwa kumpiga risasi mwandish maarufu wa habari katika mji wa Karachi.

Shambulizi hilo kwa mujibu wa idara ya polisi ni la tatu dhidi ya waandishi habari katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Aftab Alam alikuwa ni mwandishi wa habari wa eneo la kusini mwa Pakistan wa runinga ya kibinafsi ya Geo News.

Nia ya shambulizi hilo haijabainika hadi sasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wenye silaha wamemuua kwa kumpiga risasi mwandishi maarufu wa habari katika mji wa Karachi.

Jana usiku mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki alimpiga risasi na kuua fundi mitambo wa runinga hiyo hiyo ya Geo.

Dereva wa gari la kampuni hiyo anauguza majeraha.

Huko Peshawar mwandishi wa habari wa runinga ya taifa alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.