Mafuriko yazua Hofu ya njaa Sierra Leone

Image caption Chifu Gassimu Saffa wa Waima Njeila alisema mazao yao yamesombwa na mafuriko

Mafuriko yaliyotokea katika maeneo ya kusini mwa Sierra Leone yamezua hofu ya njaa na mlipuko wa maradhi yanayotokana na maji.

Kiongozi wa eneo la Bo mashariki mwa Sierra Leone katika wilaya ya Kenema amesema wakaazi 300 katika kijiji hicho wako katika hatari kubwa ya kukosa chakula.

Aidha watatbibu wanaonya kuwa huenda magonjwa ya kuambukizwa baada ya mafuriko yatazuka iwapo shughuli ya uokoaji na kupena maji masafi ya kunywa haitafanyika kwa haraka.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasemakuwa mafuriko hayo yanafuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Image caption Mafuriko yazua Hofu ya njaa Sierra Leone

Chifu Gassimu Saffa wa Waima Njeila alisema mazao yao yamesombwa na mafuriko.

Mamia ya watu bado wamekwama na hawana chakula na malazi katika sehemu ya kaskazini ya ulaya ya BO kwa siku kadhaa sasa.