Uchumi wa zimbabwe unadidimia ;IMF

Haki miliki ya picha Getty
Image caption IMF limeipongeza Zimbabwe kwa mageuzi ya kiuchumi na mipango yao ya kutatua swala la madeni

Shirika la fedha duniani IMF limesema hali ya uchumi nchini Zimbabwe imezidi kudidimia.

Aidha IMF inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi huo ni wa kiwango cha chini mno kuliko vile ilikuwa imekadiriwa.

Haki miliki ya picha afp
Image caption IMF inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi huo ni wa kiwango cha chini mno kuliko vile ilikuwa imekadiriwa

Shirika hilo la IMF limeipongeza Zimbabwe kwa mageuzi ya kiuchumi na mipango yao ya kutatua swala la madeni na taasisi za kimataifa za fedha licha ya changamoto za kiuchumi.

Hayo yametokea baada ya vuta ni kuvute baina ya serikali na sekta ya kibinafsi huku serikali ikitaka kuimarisha sekta ya uchumi na kutaifisha soko la ajira.

Haki miliki ya picha Airliners.net
Image caption Shirika la fedha duniani IMF limesema hali ya uchumi nchini Zimbabwe imezidi kudidimia.

Sekta ya kibinafsi kwa upande wake inataka kupunguza kwa gharama ya uzalishaji ilikuamabatana na hali halisi ya kiuchumi ilivyo.

Serikali ilikuwa imeruhusu kupunguzwa kwa idadi ya wafanyikazi wake lakini sekta ya umma ilipotaka kuiga mfano ikazua hofu ya kupotezwa kwa nafasi za ajira.

Rais Robert Mugabe na chama chake zanu- PF kimekuwa kikiongoza nchi ya Zimbabwe katika njia yake mwenyewe.