Wachimba madini 15 haramu wauawa AK

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa uokozi wakiwasaidia wachimba migodi haramu waliokwama chini ya ardhi

Maafisa wa polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza mauaji wa wachimba migodi 15, waliouawa wiki hii.

Wachimba migodi hao waliuawa kwa kupigwa risasi na bunduki tofauti.

Mzozo wa migodi iliyoachwa nchini Afrika Kusini katika ya makundi hasimu ya kuchimba migodi, unaendelea kuchukua sura mpya huku visa vya ghasia vikiongezeka.

Tangu mwanzo wa wiki hii wachimba migodi kumi na watano wanaojulikana kama Zama Zamas, wameuawa na polisi wanasema kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Ghasia hizo zinaonekana kuwa ishara ya kuongezeka kwa tatizo hilo, ambalo serikali na wizara ya madini inajaribu kutatua.

Wachimba migodi haramu nchini Afrika Kusini, wameishi katika migodi iliyoko chini ya ardhi kwa miezi kadhaa wakitafuta dhahabu na hivyo kumaanisha kuwa machimbo ya migodi iliyoachwa mara nyingi huvutia mzozo na mapigano kati ya makundi hasimu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachimba migodi

Mara nyingine mabomu ya kutengeneza nyumbani hutupwa ndani ya migodi hiyo na wakati mwingine hata makabiliano ya risasi,

Vitengo mbali mbali vya polisi vimetumwa katika maeneo kadhaa kukabiliana na hali hiyo.

Lakini inaonekana kuwa faida wanayopata wachimba migodi hao ni kubwa kuliko hatari wanayokumbana nayo kama vile kukamatwa au hata kuuawa wakiwa chini ya ardhi.