Silaha za kemikali zatumika Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya raia wanaodaiwa kuathirika na silaha za kemikali

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeruhusu timu ya uchunguzi kufuatilia nini nani wanaohusika mashambulizi ya silaha za Kemikali nchini Syria.

Timu hiyo wa watatu kutoka nchi wanachama na mtaalam atakayeungana nao imepewa uhuru wa kusafirik maeneo mbali mbali nchini Syria kufanya mahojiano ya uchunguzi.

Urusi na Marekani ambazo zimekuwa zikiunga mkono pande mbili tofauti katika mgogoro huo wa Syria wote wameafiki kuwepo kwa bodi hiyo mpya.

BBC umepata ushahidi unaoonyesha mashambulizi zaidi ya sitini ya silaha za kemikali kutokea nchini Syria tangu Umoja wa Mataifa ulipoagiza kuaribiwa kwa silaha za kikemikali miaka miwili iliyopita.

Majeshi ya serikali ya rais Assad na kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam IS yamekuwa yakituhumiwa kutumia silaha hizo za kikemikali.

Shuhuda wa matukio haya katika kijiji cha Maraa ameiambia BBC kwamba mashambulizi haya yanatokea upande wa kundi la Is ambao wameweka kambi karibu na kijiji hicho.

Mtalaamu wa masuala ya kemikali hatari kwa maisha ya mwanadamu ameieleza BBC kwamba bado zipo silaha hatari za kemikali na ushahidi wa dhati upo kuthibitisha madai hayo kwamba silaha hizo zimetumika kushambulia.