Wakenya 2 ICC kwa kuhonga mashahidi

Haki miliki ya picha ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imechapisha waranti ya kuwakamata wakenya wawili wanaotuhumiwa kutoa rushwa ili kuwashawishi mashahidi.

Waranti hizo juu ya Paul Gicheru na Philip Kipkoech Bett zilitolewa mwezi Machi lakini zilkuwa haziwajekwa hadi sasa.

Mahakama yasema wanaume hao walikamatwa tangu mwezi Julai.

Mwaka jana waendesha mashtaka wa ICC waliondoa mashtaka ya uhalifu wa kiubinadamu dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Lakini naibu wake,William Ruto, na mwandishi wa habari wa Kenya bado wanakabiliwa na mashtaka ya aina moja kuhusiana na vurugu zilizuka baada ya mgogoro wa uchaguzi mwaka 2007.