Baraza la Bakwata kumchagua mufti mpya

Image caption Kitabu takatifu cha Koran

Baraza kuu la Waislam nchini Tanzania, Bakwata, leo hii linafanya mkutano mkutano mkuu mjini Dodoma, huku ajenda kuu ikiwa ni kumchagua mufti mkuu mpya nchini humo.

Mufti atakayechaguliwa atakua wa tatu baada ya Hemed Bin Jumaa Bin Hemed na kufuatiwa na Mufti Issa Bin Simba, aliyefarikia dunia juni 15, mwaka huu.

Kwa sasa Sheikh Abubakari Zubery ndio anakaimu nafasi hiyo huku akiingia katika kinyanganyiro cha kuwania kuwa mufti mkuu.

Wajumbe wapatao 550 kutoka katika wilaya na mikoa nchini Tanzania watashiriki katika uchaguzi huo.