Mlipuko wa gesi wawaua watu 40 India

Haki miliki ya picha S. Niyazi
Image caption Mlipuko wa gesi waua 25 India

Polisi nchini India wanasema kuwa watu 40 waweuawa wakati mtungi wa gesi ulipolipuka katika hoteli moja iliyo jimbo la Madhya Pradesh.

Hoteli hiyo iliyokuwa karibu na kituo cha mabasi ilikuwa imejaa wafanyikazi na watoto wa shule waliokuwa wakipata kiamsha kinywa.

Waokoaji walitumia mikono yao wakiwatafuta manusura kwenye vifusi.

Majengo kadha yaliyokuwa karibu yaliharibiwa na mlipuko huo . Msemaji wa polisi anasema kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.