Sanamu ya Mau Mau kuzinduliwa Nairobi

Image caption Mau Mau

Sanamu ya makumbusho ya kundi lililopigania uhuru nchini Kenya la Mau Mau inatarajiwa kuzinduliwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi.

Sanamu hiyo ambayo itazinduliwa katika bustani ya Uhuru imelipiwa na serikali ya Uingereza ambayo imeomba msamaha kwa udhalimu wakati wa utawala wa ukoloni.

Maelfu ya watu nchini Kenya walizuiwa kambini wakati wa harakati za kundi la Mau Mau kati ya mwaka 1952 na 1960.

Sanamu hiyo inamuonyesha mwanamke akimpa chakula mpiganaji wa Mau Mau.