Wanajeshi 19 wa UG waliuawa na Alshabaab

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema kuwa wanajeshi wake 19 waliuawa kwenye shambulizi lililoendeshwa na wanamgambo wa Al shabaab nchini Somalia na wengine sita bado wakiwa hawajulikani waliko.

Museveni amewalaumu makamanda wa jeshi la Uganda kwa uzembe akisema kuwa ndiyo sababu iliosababisha kuuawa kwa wanajeshi hao wakati shambulizi lilipoendeshwa kwenye kambi ya jeshi la muungano wa Afrika eneo la Janale tarehe mosi mwezi huu.

Image caption Wanajeshi wa AMISOM

Awali Uganda ilisema kuwa ni wanajeshi 12 waliouawa.

Alshabab wanasema kuwa wanazuilia wanajeshi wa Uganda kama wafungwa wa vita.