Walipuaji wawaua watu 7 Cameroon

Haki miliki ya picha
Image caption Cameroon

Takriban watu saba wameuawa na walipuaji wa kujitolea muhanga kaskazini mwa Cameroon.

Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa Kolofata,karibu na mpaka wa Nigeria ,ambao umekuwa ukishambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram.

Mamlaka ya eneo hilo inasema kuwa watu hao watatu waliuawa katika mlipuko wa kwanza ambao ulitokea karibu na kisima karibu na mji huo, huku wengine wanne wakiuawa katika mlipuko wa pili karibu na kanisa.

Image caption Cameroon

Cameroon ni miongoni mwa mataifa yenye vikosi vya kijimbo vinavyojaribu kulikabili kundi la Boko Haram.