Mfalme wa Saudia azuru msikiti wa Mecca

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfalme Salman

Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametembelea msikiti mkubwa mjini Mecca ambapo zaidi ya watu 100 walipoteza maisha wakati kreni ilipoanguka siku ya ijumaa.

Mfalme Salman aliahidi kuwa uchunguzi utafanyika kubaini kilichosababisha ajali hiyo

Waumini waliruhusiwa kuingia eneo hilo siku ya jumamosi lakini sehemu nyingine zilisalia zimefungwa.

Maafisa wanasema kuwa sherehe za Hajj ambazo zinafanyika baadaye mwezi huu zitaendelea.