Wahamiaji:Ujerumani kudhibiti mpaka wake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji

Ujerumani inatarajiwa kuanzisha vidhibiti vya mda katika mpaka wake na taifa la Austria ili kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.

Awali msemaji wa kampuni moja ya reli kutoka Austria alisema kuwa treni zinazoelekea Ujerumani zimesitisha safari zake.

Image caption Njia inayotumiwa na wahamiaji kuingia Ujerumani

Mjini Munich pekee,zaidi ya wahamiaji 13,000 waliwasili siku ya jumamosi.

Ujerumani inatarajia wahamiaji 800,000 kuwasili nchini humo mwaka huu.

Hatahivyo bwana Maiziere hakutoa maelezo kuhusu vile vidhibiti hivyo vya mpakani vitakavyofanya kazi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ujerumani

Mwezi uliopita,alisema kuwa makubaliano ya usafiri wa viza ya Schengen ambayo huruhusu uhuru wa kutembea katika mataifa mengi ya Ulaya pia yatasimamishwa kwa mda.