Cameron azuru Lebanon

Image caption Cameron azuru Lebanon

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anazuru Lebanon ili kujionea mwenyewe namna fedha ya msaada kutoka Uingereza zinavyotumika huko.

Uingereza imetoa zaidi ya dola bilioni moja unusu ili kusaidia mamilioni ya wakimbizi katika eneo hilo.

Akizungumza katika kambi moja iliyoko katika bonde la Bekaa, chini ya nusu maili tu kutoka mpaka wa Syria, Bwana Cameron amesema kuwa msaada za Uingereza umesaidia kuwazuia mamia kwa maelfu ya raia wa Syria kutokimbilia bara Ulaya.

Haki miliki ya picha
Image caption Wakimbizi nchini Lebanon

Ametangaza uteuzi wa waziri mmoja mwenye majukumu maalum ya kushughulikia kambi za wakimbizi nchini Syria.

Uingereza imetangaza kuwa itawachukua wakimbizi elfu 20 ambao wamo hatarini katika kipindi cha miaka mitano ijayo.