Ajira zitakazochukuliwa na roboti

Image caption Roboti

Je, Teknolojia imekuwa ikichukua kazi za mikono kwa miaka kadhaa sasa?Lakini ni kazi gani ambazo roboti itazinyakua katika miaka ya baadaye.

Takriban asilimia 35 ya ajira nchini Uingereza zipo katika hatari ya kuchukuliwa na teknolojia ya tarakilishi katika kipindi cha miaka 20 ijayo kulingana na utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Oxford na Deloitte.

Tafuta kazi yako ili ujue iwapo huenda ikatekwa kiteknolojia katika kipindi cha karne mbili zijazo.

Wasomi katika chuo kikuu cha Oxford Michael Osborne na Carl Frey walifanya utafiti wa ni vipi ajira zipo katika athari ya kutekwa na teknolojia katika vigezo vitisa.

Uwekevu kijamii, majadiliano, ushawishi, kusaidia na kutunza wengine, uhalisi, sanaa ,ustadi, mwongozo wa ustadi na haja ya kufanya kazi katika nafasi duni.

Utafiti huo ulifanywa kwa kutumia data ya kazi yenye maelezo kamilifu.

Baadhi ya kazi ambazo ziko katika harati ya kuchukuliwa na Roboti ni zile za madereva wa texi,waandishi wa habari,kazi za viwandani,zile za madaktari na wahudumu wa mikawa

Madereva wa texi katika miji mingi duniani kwa sasa wanazozana na kampuni ya texi ya Ubber kwa huduma ambazo madereva wa gari hizo hawapewi.

Haki miliki ya picha b
Image caption Gari la roboti linaloweze kujiendesha bila dereva

Hatahivyo Ubber pamoja na kampuni nyingi za magari wanatafuta mbinu ambapo wataweza kuendesha magari yao bila maderava hao.

Nchini Uchina binaadamu wanatengeza roboti ambazo zitachukua kazi zao.

Kiwanda cha kwanza ambacho roboti ndio watakuwa wafanyikazi kinajengwa katika kiwanda cha Dongguan nchini Uchina.

Image caption Kiwanda cha roboti

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Shenzen Evenwin kinalenga kupunguza idadi ya ajira zilizopo 1,800 kwa asilimia 90,kulingana na Chen Zingui,mwenyekiti wa bodi.

Iwapo umeweza kusoma ripoti ya malipo katika makampuni ndani jarida la forbes ama habari ya michezo katika chombo cha habari cha AP basi ujue kwamba iliandikwa na Roboti.

Kampuni kama vile Narrative science hutoa programu kama ile ya Quill ambayo ina uwezo wa kuchukua data na kuibadilisha na kuwa kitu kinachoeleweka.

Image caption Waandishi wa habari

Quill huandika ripoti za makampuni kabla ya tangazo la mapato, na kampuni ya Narrative Science inadai kwamba hatua hiyo inamaanisha kwamba jarida la Forbes sasa lina uwezo wa kutoa ripoti kama hizo kwa maelfu ya makampuni badala ya habari chache ambazo huandikwa na waandishi wa habari.

Mwanasayansi mkuu katika kampuni ya Narrative science Kristian Hammond awali amenukuliwa akisema kuwa katika kipindi cha miaka 15 ijayo asilimia 90 ya ajira katika sekta ya habari zitachukuliwa.

Haki miliki ya picha st josephs healthcare
Image caption Roboti katika upasuaji

Roboti huenda haina tabia nzuri lakini ina uwezo kuingia katika mkusanyiko wa data ili kutafuta tiba ya ugonjwa fulani.

Kampuni ya IBM kwa sasa inashirikiana na hospitali nyingi nchini Marekani,ili kutoa ushauri kuhusu tiba nzuri kwa magonjwa kadhaa ya saratani.

Kwa kutumia programu zinazoweza kuona zilizotengezwa na kampuni hiyo, inasaidia kugundua visa vya mapema vya saratani ya ngozi.

Na roboti kwa mda mrefu zimekuwa zikiwasaidia madaktari kufanya upasuaji katika wakfu wa hospitali ya Guys and St Thomas,kwa mfano roboti huwasaidia madaktari katika upasuaji wa figo.

Haraka ,ni kigezo muhimu katika ufanisi wa upasuaji na roboti huweza kushona mishipa ya damu inayoshikana na figo mpya ikilinganishwa na binaadamu.

Image caption Bar ya roboti

Meli ya kitalii kutoka visiwa vya Caribean kwa jina Anthem hivi majuzi ilianzisha baa ya roboti kwa jina Shakr Makr.

Vinywaji vinaweza kuitishwa kupitia tarakilishi na wateja wana uwezo wa kubuni orodha ya vyakula wanavyotaka.

Ninatumaini kwamba walimu na majaji wataendelea kuwa binaadamu kwa sababu mara kwa mara utahitaji mtu wa kuzungumza naye,kulingana na Nello Cristianini ambaye ni profesa katika chuo kikuu cha Bristol.

Hatahivyo kazi tunazofanya zinashirikisha mawasiliano ya kuzungumza kuhusu utendekazi na hata iwapo ni muhimu kutengeza roboti zinazozungumza haitafanyika hivi karibuni.