Wahamiaji:Mawaziri wa Ulaya wakutana

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ulaya

Mawaziri wa sheria na mambo ya ndani kutoka nchi za Ulaya wanafanya mkutano wa dharura kuzungumzia tatizo la uhamiaji.

Mawaziri hao wanajadili mpango wa kuwapa hifadhi wahamiaji elfu mia moja ishirini katika nchi za umoja wa Ulaya.

Ufaransa na Ujerumani zinashinikiza kuwepo kwa ugawanaji sawa wa wakimbizi na pia ratiba ya utekelezaji mpango huo.

Hatahivyo baadhi ya nchi za katikati mwa Ulaya zikiwemo Poland,Hungary Slovakia na jamuhuri ya Chek zinapinga mpango huo.

Mataifa haya yanadai kuwa hatua hiyo itawavutia wahamiaji zaidi kuelekea Ulaya.