Upinzani waitisha maandamano DRC

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Upinzani DRC

Vyama kadhaa vya upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimeitisha maandamano katika mji mkuu wa taifa hilo Kinsasha dhidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliotarajiwa mwezi Novemba mwaka 2016.

Wiki iliopita ,mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kuangaziwa upya ,hatua ambayo wapinzani wanasema ni ya kutaka rais Joseph Kabila kusalia mamlakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba.

Mabango yaliobebwa na vyama hivyo yalisoma ''mabadiliko ya uongozi ni sharti yafanyike''.

Haki miliki ya picha
Image caption Drc

Maandamano ya kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi huo yalizua ghasia mnamo mwezi Januari na kusababisha vifo vya takriban watu 36.

Bwana Kabila amekuwa madarakani tangu babaake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka 2001.