'Mti wa wageni' uwanja wa ndege wa Kismayu

Haki miliki ya picha
Image caption Kismayu

Iwapo umezoea kuwasili katika maeneo yaliotengewa wageni wanaowasili katika viwanja vya ndege vya kimataifa, basi pengine ungetembea kusini mwa Somalia katika mji wa Kismayu.

Badala ya kuwepo kwa eneo lililotengewa wageni wanaowasili, kuna mti uliotengewa wageni hao, ambapo wiki hii wajumbe walioelekea nchini humo kwa mazungumzo walikaribishiwa kabla ya kupelekwa katika hoteli wanakotakiwa kulala.

Mohammed Abdi Affey (wa pili kutoka kulia pichani) ambaye ni mjumbe wa Shirika la Igad nchini Somalia aliiambia BBC vile alivyojisikia kuhusu utamaduni huo.

''Hakuna heshima kubwa kama kukaribishwa chini ya mti katika uwanja wa ndege ambao una kivuli kizuri. Tunafurahia sana mti huu wa wageni''.