Utafiti:Tarakilishi husababisha matokeo mabaya shuleni

Haki miliki ya picha Sean Gallup Getty Images
Image caption Utumizi wa tarakilishi miongoni mwa wanafunzi

Ripoti mpya kutoka shirika la OECD inasema kuwekeza kwenye kompyuta mashuleni hakuleti kiwango kikubwa cha mabadiliko ya matokeo kwa wanafunzi darasani.

Utafiti huu unatolewa huku mradi wa kila mtoto kupewa kompyuta darasani ukisifiwa kama hatua kubwa ya kusaidia kurahisishia wanafunzi kuendeleza masomo yao.

Kulinagana na shirika hilo utumizi wa mara kwa mara wa tarakilishi husababisha kuwepo kwa matokeo mabaya.

Mkurugenzi wa OECD Andreas Schleicher anasema kuwa teknolojia katika shule imezua matumaini ya uongo.

Image caption Utafiti wa tarakilishi shuleni

Mtaalam wa maswala ya tabia za wanafunzi nchini Uingereza Tom Bennet amesema kuwa walimu wanadanganywa na tarakilishi mashuleni.

Ripoti hiyo kutoka kwa shirika la muungano wa kiuchumi na maendeleo iliangazia athari za teknolojia shuleni katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kama vile ile ya pisa inayofanywa katika zaidi ya mataifa 70 pamoja na mitihani ya kukagua viwango vyo kidijitali.

Inasema kuwa mifumo ya elimu ambayo imewekeza pakubwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano haijaimarishwa katika mitihani ya pisa ya masomo ya kusoma,hesabati na sayansi.

''Ukiangalia mifumo inayofanya vyema kama ile ya mashariki mwa Asia,imekuwa ikitumia teknolojia katika madarasa yao na tahadhari kubwa alisema'', Schleicher.

Image caption Utafiti wa tarakilishi katika komputer

Wale wanaotumia vipatakilishi na tarakilishi mara nyingi hupata matokeo mabaya ikilinganishwa na wale wanaotumia kwa kadri.

Matumizi katika sekta ya elimu duniani hugarimu pauni bilioni 17 kulingana na mchanganuzi wa maswala ya teknolojia Gartner.

Nchini Uingereza, matumizi kuimarisha sekta ya teknolojia katika mashule ni pauni milioni 900.

1.Wanafunzi wanaotumia tarakilishi mara kwa mara katika shule hupokea matokeo mabaya.

2.wanafunzi wanaotumia tarakilishi katika shule kwa kadri,kama vile mara moja ama mbili kwa wiki hupata matokeo mazuri ikilinganishwa na wanafunzi wanaotumia tarakilishi kila mara.

3.Matokeo hayo hayaonyeshi matokeo mazuri katika masomo ya kusoma,hesabu na sayansi katika mataifa ambayo yamewekeza kwa kiwango kikubwa katika teknolojia ya habari.

4.Shule zilizo na mifumo ya matokeo mazuri kama vile Korea Kusini na Shanghai nchini Uchina zina matumzi ya chini ya tarakilishi.

5.Taifa la Singapore ambalo shule zake hutumia tarakilishi kwa kadri linaongoza katika uwezo wa kidijitali