Wahamiaji: Mataifa ya Ulaya yatofautiana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wa Ulaya

Naibu Chansela wa Ujerumani ameelezea ghadhabu zake kutokana na hatua ya mawaziri wa muungano wa Ulaya kushindwa kukubaliana kuhusu mpango wa kugawana wahamiaji.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin Sigmar, Gabriel amesema Ulaya imejiaibisha tena baada ya mawaziri wa mataifa ya katikati mwa bara hilo kupinga mpango wa kuipa hifadhi idadi kubwa ya wahamaiaji ambao tayari wamewasili barani humo.

Awali waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani alisema muungano wa Ulaya unapaswa kuwaondoa nchi wanachama ambao wamepinga mpango huo.

Mawaziri hao watakutana tena wiki tatu zijazo kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mpango huo.