Je, wajua 'Mbuzi' ni jina la utani la rais wa Ghana

Image caption John Mahama

Moja la bango lililokuwa limebebwa na waandamanaji hii leo katika mji wa Accra nchini Ghana huenda likaonekana kama lenye ujumbe m'baya kwa mtu asiyeelewa.

Wanasema kuwa majina ya watu wasiokuwepo katika sajili ya wapiga kura huenda yakampigia kura rais huyo.Alipata jina hilo la utani baada ya kusema kuwa ana tatizo la mbuzi waliokufa.

Image caption Mbuzi

''Nimeona maandamano mengi na migomo katika kipindi changu cha miaka miwili madarakani.Sidhani kwamba inaweza kuwa zaidi ya hiyo.Inasemekana kwamba unapoua mbuzi na kuitishia na kisu,haiogopi tena kisu kwa sababu tayari imekufa''.Joy Online alimnukuu rais huyo akizungumza mnamo mwezi Machi.

Kwa hivyo nchini Ghana hata mtoto mdogo anajua kuwa jina la rais la utani ni Mbuzi.