Serbia yailaumu Hungary kuhusu wakimbizi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakimbizi wakishambuliwa kwa mabomu ya machozi

Serbia na Umoja wa mataifa wameilaumu Hungary kwa kitendo cha kupiga mabomu ya machozi ili kuwazuia wakimbizi wanaotaka kuingia kaskazini mwa bara la ulaya.

Waziri mkuu wa Serbia, Aleksandar Vucic , ameishutumu Hungary kwa kuwa wakatili kwa raia wasiotoka bara la Ulaya.

Wakati katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ameshangazwa na jinsi ambavyo wakimbizi hao wamekuwa wakifanyiwa.

Ingawa Hungary ilijitetea kwa kudai kuwa baadhi ya askari wao walijeruhiwa wakati wakiwazuia wakimbizi hao kufanya ghasia huku wakijaribu kupita kwenye uzio wa seng'enge iliyokuwa imewekwa kuwazuia kupita.