Wahamiaji wapata njia mpya Croatia

Haki miliki ya picha RENGIN ARSLAN
Image caption Wahamiaji wa Syria

Kundi la kwanza la wahamiaji limewasili nchini Croatia ,ambayo ni njia mpya ya kuelekea mataifa ya Ulaya yaliopo kaskazini ,siku moja baada ya Hungary kufunga mpaka wake na Serbia.

Takriban wahamiaji 150 walivuka na kuingia katika mataifa ya muungano wa Ulaya kutoka Serbia.

Croatia inasema kuwa iko tayari kuwapokea moja kwa moja ama kuwaelekeza kule wanakotaka kwenda.

Wahamiaji wengi kutoka Syria wana matumaini ya kuelekea Ujerumani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji

Masharti mapya yaliowekwa katika mipaka pamoja na mzozo kuhusu kugawana maelfu ya wahamiaji hao kumezua tofauti kubwa miongoni mwa mataifa ya Ulaya.

Mamia ya wahamiaji waliokwama walingojea nje usiku kucha ama katika mahema karibu na mpakawa Serbia na Hungary.