Ndege yaahirisha safari kuokoa mbwa

Haki miliki ya picha CityNews Toronto
Image caption Mbwa aliyeokolewa

Safari ya Ndege iliyokuwa ikielekea Toronto Canada siku ya jumapili ilielekezwa Frankfurt nchini Germany kwa ghafla, baada ya rubani kugundua kuwa kifaa kinachoweka joto katika chumba cha kubeba mizigo kilikuwa hakifanyi kazi huku maisha ya mbwa aliyekua ndani yakiwa hatarini.

Mbwa huyo anaye tambulika kama lion ana miaka saba na alikua ndani ya chumba hicho.Bila joto kitengo hicho kinaweza kuwa baridi sana kutokana na urefu ambao ndege hiyo imepaa .

Hali hiyo inaweza kusababisha kifo. Ndege hiyo ilioyotoka Tel Aviv,Israel,na kuelekea Toronto Canada ilielekezwa Mjini Frankfurt Ujerumani. Takriban abiria 200 walicheleweshwa kwa dakika sabini na tano ili kuokoa maisha ya mbwa huyo.

Bwana Fitzpatrick alisema kuwa ijapokuwa kifaa hicho cha kuweka joto katika chumba cha mizigo sio muhimu katika safari ya ndege hiyo ,rubani aliamua kuelekea Ujerumani wakati ambapo ndege hiyo ilikuwa inaelekea katika bahari ya Atlantic ili kuokoa maisha ya mnyama huyo.

Mjerumani Kontorovich ambaye ni mmiliki wa mbwa huyo alimshukuru rubani kwa kusulihisha tatizo hilo kwa haraka. Bwana Kontorovich aliambia wanahabari wa chombo cha habari cha Canadian City News kuwa mbwa huyo ni kama mtoto wake na anampenda sana.